Aliyekuwa Jaji Mkuu David Maraga amesisitiza umuhimu wa Wakenya wanaoishi nje ya nchi katika kukuza uchumi wa taifa kupitia michango yao. Akizungumza na Wakenya jijini Dallas, Texas, Maraga alisema kuwa Wakenya wanaoishi nje ni wadau muhimu ambao mchango wao wa kiuchumi hauwezi kupuuzwa. Maraga, ambaye anawania urais, alitoa wito wa kutambuliwa zaidi kwa Wakenya hawa na mchango wao katika maendeleo ya taifa.
DAVIDA MARAGA – DIASPORA