Wakaazi wa Kaunti ya Nyeri wanapaswa kutarajia mvua kubwa kesho, amesema Mkurugenzi wa Huduma za Hali ya Hewa katika Kaunti hiyo, Peter Wambugu. Wambugu alisema mvua hiyo, ambayo ni sehemu ya mvua za vuli (ya miezi ya Oktoba, Novemba na Disemba), itaongezeka katika siku zijazo. Aliwahimiza wakulima kushauriana na maafisa wa nyanjani wa kilimo katika maeneo yao kuhusu wakati mwafaka wa kupanda mazao.