Baadhi ya wabunge wanashinikiza kufanyiwa marekebisho kwa sheria za pensheni ili kuweka adhabu kwa waajiri wanaokata michango ya pensheni kutoka kwenye mishahara ya wafanyakazi lakini wakashindwa kuwasilisha fedha hizo kwenye hazina husika. Wakati wakijadili taarifa za fedha zilizokaguliwa za hazina tano, ikiwemo hazina ya Usawazishaji (Equalization Fund), wabunge hao walisema kuwa kutowasilishwa kwa fedha hizo kunawafanya wastaafu kupata changamoto katika kupata fedha zao. Walibainisha kuwa hali hii inaendelea licha ya agizo la Rais linalotaka malipo ya wastaafu yakamilishwe ndani ya siku 10 tangu kustaafu.
KAGUCHIA SIYOI – PENSION