Naibu Rais Kithure Kindiki amesema kuwa pombe haramu sasa imeorodheshwa miongoni mwa vitisho vikubwa zaidi dhidi ya kuwepo kwa taifa la Kenya, na kwamba hatua kali zaidi zinawekwa ili kukomesha tatizo hilo. Kutokana na kuorodheshwa huko, Kindiki amesema ofisi yake inaratibu mkakati wa kitaifa ili kuhakikisha kuwa hatua hizo mpya zinafanikiwa. Akizungumza katika makaazi yake huko Karen, Kindiki alisisitiza kuwa kampeni hii si shambulio dhidi ya biashara halali au sekta husika, bali ni jitihada za kulinda taifa lisije likaporomoka.

KITHURE KINDIKI - YOUNG