Timu ya 'Junior Starlets', inalenga kuonyesha kiwango bora zaidi dhidi ya Marekani katika mechi yao ya pili wa Kombe la Dunia la FIFA la Wanawake la U-17, linalofanyika Rabat, Morocco, usiku wa leo. Starlets walipoteza 3-0 dhidi ya China katika mechi ya ufunguzi Jumatatu, na sasa wanahitaji kucheza kwa ubora wa juu ili kupata angalau pointi moja dhidi ya Marekani, timu ambayo iliichapa Samoa mabao 17-0 katika mechi yao ya kwanza. Kocha Mkuu wa Starlets, Mildred Cheche, anasema washambuliaji wake wanapaswa kuwa makini zaidi na hodari katika kufunga mabao ikiwa Kenya inataka kushindana na Marekani, ambao wanatazamwa kama moja ya timu za juu.

Kocha Mkuu wa timu ya wavulana ya Kenya ya U-15, Patrick Nyale, anaamini kuwa wamejiandaa vyema kwa ajili ya mashindano ya kwanza kabisa ya Kombe la Dunia la FIFA la U-15 yatakayofanyika Baku, Azerbaijan, na anatarajia matokeo mazuri. Katika hatua ya awali ya mashindano hayo, Kenya imepangwa kundi moja na Malta, Chad, Niger, Panama, na North Macedonia. Mashindano haya yatatumia mfumo wa kipekee ambapo kila timu itakuwa na wachezaji 8 uwanjani, wakicheza kwenye viwanja vilivyopunguzwa ukubwa, vyenye vipimo vya mita 68 kwa 50. Jana, Nyale alitangaza kikosi cha wachezaji 14 kabla ya safari yao.

PATRICK NYALE - U-15

Jua linashuhudiwa Nairobi, Kajiado na Narok.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.