Mpango wa uhifadhi wa Thamani Asili unalenga zaidi ya ajira elfu 20 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja huku ukinufaisha takriban watu milioni 1.6 kote nchini. Mpango huo, uliozinduliwa katika Hifadhi ya Kitaifa ya Tsavo Magharibi, utasaidia zaidi ya hifadhi 130 za jamii katika mandhari nne za kipaumbele. Mkurugenzi Mkuu wa KWS Erustus Kanga anasema ushiriki wa jamii, riziki endelevu na suluhisho za vitendo kwa migogoro ya binadamu na wanyamapori zitakuwa muhimu katika utekelezaji wake.
ERUSTUS KANGA – PROGRAM