Kiongozi wa PLP, Martha Karua, amemshauri aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua asifunge mlango kwa kiongozi yeyote wa upinzani, huku juhudi za kuunganisha upinzani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027 zikishika kasi. Karua alimwonya Gachagua dhidi ya kuwapuuza washirika watarajiwa, akisisitiza kuwa hakuna kiongozi anayepaswa kuonekana mbaya zaidi kuliko mwingine bila kufanyiwa tathmini. Alitoa wito wa umoja na mtazamo unaojumuisha wote katika siasa za upinzani.
MARTHA KARUA – OPPOSITION