Naibu Rais Kithure Kindiki anasema masoko mapya yanayojengwa chini ya ajenda ya serikali ya mageuzi ya kiuchumi yatawapa wafanyabiashara zaidi ya nafasi za kuuza. Vifaa hivyo vitajumuisha hifadhi ya baridi, migahawa, vyumba vya akina mama, maeneo ya kuchezea watoto na vituo vya ICT ili kusaidia biashara ya mtandaoni na kazi za kidijitali. Huko Gatundu North, Kindiki anasema masoko ya Kamwangi na Gatukuyu pia yanakaribia kukamilika, kwa gharama ya shilingi milioni 387 na milioni 56, mtawalia.

KITHURE KINDIKI – MARKETS