Polisi wamewakamata washukiwa wawili katika operesheni tofauti katika kaunti za Kiambu na Embu, na kufanikiwa kunasa misokoto 1,087 vinavyodhaniwa kuwa ni bangi. Huko Juja, Kaunti ya Kiambu, maafisa walimkamata mwanamke mmoja na kunaza misokoto 800, huku mshukiwa wa pili akikamatwa Embu akiwa na misokoto 287. Washukiwa wote wawili wanazuiliwa na polisi wakisubiri kufikishwa mahakamani, huku uchunguzi ukiendelea.