Seneta wa Kakamega, Boni Khalwale, anasema Seneta wa Nairobi, Edwin Sifuna, ndiye mwenye uamuzi wa mwisho kuhusu chama cha kisiasa atakachotumia katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027 chini ya vuguvugu la 'Linda Mwananchi'. Kauli hii inakuja wakati Sifuna akitarajiwa kuzindua chama chake mapema mwezi ujao. Akizungumza katika kipindi cha asubuhi cha runinga ya NTV, Khalwale alisema Sifuna aliidhinishwa kwa kauli moja kuwa mgombea urais wa vuguvugu hilo na ataongoza mazungumzo na vyama vya kisiasa pamoja na viongozi wenye mtazamo sawa kabla ya uchaguzi wa 2027.


BONI KHALWALE –FINAL