Wizara ya Afya imewataka Wakenya kuwa watulivu, kuzingatia hatua za afya ya umma na kutegemea njia rasmi kupata taarifa sahihi kufuatia kuthibitishwa kwa kisa cha Ebola nchini. Jopo kazi la Kitaifa la Mashirika Mbalimbali kuhusu Ebola, likiongozwa na Katibu wa Afya ya Umma Mary Muthoni, lilipitia hatua za kudhibiti ugonjwa huo asubuhi ya leo, likizingatia zaidi usimamizi wa wagonjwa, uhamasishaji wa rasilimali, vituo vya kutengwa kwa wagonjwa na ulinzi wa wahudumu wa afya walio mstari wa mbele ili kuzuia maambukizi zaidi.