Wakenya wametakiwa kuzingatia tabia za lishe bora na kufanya mazoezi mara kwa mara ili kupunguza hatari ya kupata magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanayotokana na mtindo wa maisha. Wito huo umetolewa kufuatia zoezi la uchunguzi wa afya lililofanyika Mwea, Kaunti ya Embu, ambapo visa vya ugonjwa wa kisukari na shinikizo la juu la damu viligunduliwa miongoni mwa wakaazi. Mkuu wa Huduma za Afya ya Msingi katika Kaunti hiyo, Mercy Wanjala, aliwahimiza Wakenya kukumbatia lishe bora na mazoezi, akibaini kuwa magonjwa haya yanaweza kuzuilik.

MERCY WANJALA-WATCH