Rais William Ruto amewapa changamoto wapinzani wake wa kisiasa kuwasilisha mawazo mbadala ya kuendeleza nchi, badala ya kupinga miradi yake mikuu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027. Akizungumza katika sherehe za Siku ya Mashujaa mjini Eldoret, Rais aliwahimiza Wakenya kukataa migawanyiko ya kikabila na siasa za kurudisha nyuma maendeleo, akisisitiza kuwa ushindani wa kisiasa unapaswa kujikita katika ajenda za maendeleo na suluhisho halisi, badala ya siasa zinazotegemea misingi ya kikabila.

WILLIAM RUTO-PRESENT