Walimu nchini wamehimizwa kuweka kipaumbele katika afya yao ya akili na kutafuta huduma za ushauri nasaha, kufuatia wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa visa vya kujitoa uhai na matumizi mabaya ya pombe. Viongozi wa vyama vya walimu vya KUPPET na KNUT katika eneo bunge la Ndaragwa waliwahimiza walimu kuzungumzia changamoto wanazopitia na watu wanaowaamini, kutafuta msaada kutoka kwa wataalamu, na kusimamia mishahara yao kwa busara ili kukabiliana na changamoto za kibinafsi na za kifedha.

VOX POP-PRIORITIZE