Viongozi wanaounga mkono serikali katika eneo la Pwani wamewahimiza wakaazi kumchagua tena Rais William Ruto mwaka ujao, wakitaja rekodi ya maendeleo ya serikali yake. Wakiongozwa na Waziri wa Madini Hassan Joho pamoja na Gavana wa Mombasa Abdulswamad Nassir, viongozi hao waliipongeza serikali kwa kushughulikia dhuluma za kihistoria za ardhi ambazo zimeathiri jamii za eneo hilo kwa miaka mingi. Pia walionyesha miradi ya maendeleo inayoendelea katika eneo hilo, ambayo walisema inadhihirisha dhamira ya serikali ya kuboresha maisha ya wakaazi.

VOX POP-ELECT