FKF imeanzisha mchakato wa kuitisha Mkutano Mkuu Maalum kwa lengo la kuwaondoa wajumbe wa Kamati yake ya Kitaifa ya Utendaji ambao wanapinga uongozi. Shirikisho hilo limesambaza fomu za hati za kiapo kwa matawi na klabu ili zisainiwe, likilenga kupata uungwaji mkono unaohitajika kuitisha mkutano huo—ambao unaweza kufanyika ndani ya wiki mbili zijazo iwapo idadi inayohitajika itapatikana. Ili kuitisha Mkutano Mkuu Maalum, FKF inahitaji saini kutoka kwa robo tatu ya wajumbe 92, idadi ambayo ni sawa na wajumbe 69.
Jua linashuhudiwa Makindu, Mtito a ndei na Voi.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.