Maafisa wa upelelezi wamenasa shehena ya Cocaine yenye thamani ya takriban Shilingi milioni 2.19 wakati wa ukaguzi wa kawaida wa abiria na mizigo katika Kituo cha Pamoja cha Mpakani cha Malaba. DCI imesema kuwa operesheni hiyo ilisababisha kukamatwa kwa mtuhumiwa mmoja, baada ya maafisa kugundua kifurushi kilichokuwa ndani ya basi la abiria lililokuwa likitoka Kampala kuelekea Nairobi. Kulingana na DCI, kifurushi hicho kilizua shaka wakati wa ukaguzi wa kawaida, jambo lililopelekea maafisa kukifanyia uchunguzi wa kina zaidi.