Chama cha Wafanyakazi wa Vyuo Vikuu nchini (KUSU) kimetishia kuendeleza mgomo wake hadi mwaka ujao iwapo serikali itashindwa kushughulikia madai yake. Katibu Mkuu Charles Mukhwaya anasema chama hicho kitakataa makubaliano yoyote yanayodhoofisha ustawi wa wanachama wake, huku akionya kuwa mgomo wa muda mrefu unaweza kuwashawishi wapiga kura kuiondoa madarakani serikali ya sasa. Mazungumzo kati ya wahadhiri na serikali yalikwama siku tisa zilizopita, huku mgomo huo ukivuruga shughuli za masomo na sekta ya elimu kwa ujumla.