Katibu Mkuu katika Wizara ya Mambo ya kigeni, Korir Sing’oei, ametetea uamuzi wa Marekani wa kubadilisha ushauri wake wa usafiri kwa Kenya, akibaini kuwa nchi hiyo ina wajibu wa kutoa ushauri kwa raia wake. Akijibu wasiwasi kuhusu kuwekwa kwa Kenya katika kundi la tatu kufuatia visa tisa vya ugonjwa wa Ebola, Sing’oei alisisitiza kuwa ushauri huo hauna maana ya kupiga marufuku safari. Alisisitiza kuwa ushirikiano wa kimataifa katika afya ya umma na ufuatiliaji thabiti mipakani bado ni mambo muhimu sana.

KORIR SING’OEI – US