Kutangaza matokeo ya uchaguzi moja kwa moja ni sehemu kubwa ya kujenga uaminifu katika mfumo wa uchaguzi, hii ni kulingana na Katibu Mkuu wa Mambo ya kigeni Korir Sing’oei. Sing’oei alikiri mapengo ya kiteknolojia na wasiwasi wa usalama wa mtandao, lakini akasema kwamba masuala hayo yanapaswa kutatuliwa badala ya kutumika kuondoa utangazaji wa moja kwa moja. Uungaji mkono wake wa kuweka matokeo ya moja kwa moja unakuja huku kukiwa na mjadala kuhusu Muswada wa Marekebisho ya Uchaguzi.

KORIR SING’OEI – STREAMING