Katibu wa Afya ya Umma Mary Muthoni amewasihi Wakenya kuwa watulivu na makini kufuatia uthibitisho wa kisa cha Ebola nchini, akiwahakikishia kwamba hakuna mkurupuko au sababu ya tahadhari. Alisema serikali inaratibu ufuatiliaji na uchunguzi katika sehemu zote za kuingilia, huku watu walioingiliana na mgonjwa wakitengwa kama tahadhari. Muthoni aliwasihi umma kuendelea na shughuli za kawaida na kutegemea taarifa zilizothibitishwa kutoka Wizara ya Afya.

MARY MUTHONI-CALM