Naibu Rais Kithure Kindiki anasema serikali inaimarisha miundombinu ya usafirishaji kupitia ujenzi wa barabara mpya kote nchini. Akizungumza mjini Othaya, Kaunti ya Nyeri, Kindiki alisema serikali ya Kenya Kwanza imejenga kilomita 775 za barabara katika Kaunti ya Nyeri kwa gharama ya shilingi bilioni 45. Aliongeza kuwa masoko 13 ya kisasa yamejengwa katika kaunti hiyo ikiwa ni sehemu ya mpango wa serikali wa kujenga masoko 600 nchi nzima.


KITHURE KINDIKI-NYERI