Rais William Ruto ametangaza mipango ya serikali kuu kuchukua jukumu la kusimamia hospitali za rufaa za Kakamega na Garissa, na kuzipandisha hadhi kutoka vituo vya Level 5 hadi Level 6. Akizungumza mjini Kakamega, Rais alisema serikali kuu itagharimia uendeshaji wa hospitali hizo, hatua itakayowezesha serikali za kaunti hizo mbili kuelekeza rasilimali zao katika ujenzi wa hospitali nyingine za Level 5.


WILLIAM RUTO-HOSPITALS