Gavana wa Trans Nzoia, George Natembeya, amepuuza madai ya Rais William Ruto kwamba siasa za vuguvugu lake la ‘Tawe’ zinakwamisha maendeleo katika kaunti hiyo. Natembeya alisema wakaazi wana haki ya kikatiba ya kupata maendeleo na hawapaswi kuchukuliwa kama watu wanaopewa upendeleo wa kisiasa, akisisitiza kuwa wao hulipa kodi kama Wakenya wengine. Alimtuhumu Ruto kwa kumshambulia kutokana na msimamo wake wa upinzani.


GEORGE NATEMBEYA –POLITICS