Mkuu wa utumishi wa umma Felix Koskei ametoa wito wa kuimarishwa kwa maandalizi na ufuatiliaji mkali zaidi mipakani ili kuzuia kuenea kwa Ebola. Koskei aliwataka maafisa kulichukulia suala hilo kwa uzito, akionya kuwa ugonjwa huo unaweza kusababisha vifo iwapo hautadhibitiwa. Pia alionya dhidi ya kuingiza siasa katika juhudi za kukabiliana na hali hiyo, akisisitiza umuhimu wa hatua za pamoja ili kulinda afya ya umma.
FELIX KOSKEI – EBOLA
Read Also
Koskei pia amewataka maafisa wa serikali kuhakikisha kuwa mvua inayotarajiwa ya El Niño haivurugi mitihani ya kitaifa.