Kuna uhaba wa kutisha wa wauguzi waliobobea katika kuwahudumia wazee, jambo linalosisitiza hitaji la kuwepo kwa wafanyakazi zaidi waliofunzwa kutoa huduma za afya nchini. Hili lilibainika wakati wa hafla ya kufuzu katika Chuo cha Mafunzo cha Mercy Life kilichoko Kiambu, ambapo wasiwasi ulionyeshwa kuhusu ongezeko la tishio la magonjwa kwa wazee ikilinganishwa na miaka ya nyuma. Wahitimu walipata ujuzi wa kivitendo katika utoaji huduma za afya majumbani na hospitalini, huku mkurugenzi Rosemary Nyambura akisema kuwa mtaala wa mafunzo hayo unakidhi viwango vya kimataifa.

ROSEMARY NYAMBURA-CARE