Mke wa Kiongozi wa DCP Rigathi Gachagua,  Dorcas Rigathi, ameeleza wasiwasi wake kuhusu kuongezeka kwa visa vya ulevi na matumizi mabaya ya dawa za kulevya, hasa katika eneo la Mlima Kenya. Akizungumza huko Marekani, Dorcas alilaumu uzembe wa serikali kwa hali hiyo. Alionya kuwa matumizi mabaya ya dawa za kulevya miongoni mwa vijana, wakiwemo wanafunzi wa vyuo vikuu, yanahatarisha maisha yao ya baadaye na akatoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka ili kukabiliana na janga hilo.


DORCAS RIGATHI-ABUSE