Mshukiwa wa mauaji Rose Mbithe na wanawe wawili watabaki kizuizini wakisubiri uamuzi kuhusu ombi lao la dhamana. Mbithe amewasilisha ombi jipya la kumhoji mumewe wa zamani, David Ndetei, kuhusu hati ya kiapo inayopinga kuachiliwa kwao. Jaji wa Mahakama Kuu ya Milimani, Alexander Muteti, ameahirisha kikao cha kusikilizwa kwa dhamana hadi Oktoba 19. Mbithe na wanawe wanashtakiwa kuhusiana na mauaji ya mtafiti wa afya ya akili Victoria Mutiso.


ALEXANDER MUTETI – PROCEEDINGS