Rais wa CAF, Patrice Motsepe, jana alithibitisha kuwa viongozi wa soka barani Afrika wataunga mkono kwa kauli moja kugombea tena kwa Gianni Infantino nafasi ya urais wa FIFA katika uchaguzi wa mwaka ujao. Katika taarifa ya pamoja, vyama vyote 54 wanachama kutoka Afrika vilionyesha uungaji mkono wao kwa Infantino wakati wa mkutano wa Mkakati wa CAF uliofanyika Cape Verde. Uungaji mkono huo unakuja licha ya mashirikisho ya maeneo mengine kama Ulaya na Marekani Kaskazini kupinga uongozi wa Infantino kufuatia jaribio lake lililoshindwa na kuzua utata la kubinafsisha Kombe la Dunia. Motsepe pia alihimiza kuendelezwa kwa uwekezaji katika kukuza vipaji vya vijana na vituo vya mafunzo ili kuinua kiwango cha soka barani Afrika.
PATRICE MOTSEPE - GIANNI
Kenya itakuwa na timu tano katika mashindano ya mwaka huu ya Safari7s yanayoanza jioni hii katika Uwanja wa Nyayo. Timu za wanaume zitakuwa mbili, Shujaa na Morans, huku upande wa wanawake ukishiriki na timu tatu: Lionesses, Shibli na Junior Lionesses. Kenya Morans itachuana na kikosi cha GEL saa kumi unusu jioni, huku Shujaa ikimenyana na Sportpesa Legends saa kumi na moja na dakika 56 jioni katika raundi ya kwanza ya mechi, kabla ya kutoa nafasi kwa raundi ya pili kesho. Hatua ya mtoano itafanyika siku ya Jumapili.
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Nairobi, Narok na Kajiado.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.