Kocha Mkuu mpya wa Harambee Starlets, Godfrey Oduor, anasema watawapa wachezaji wapya fursa ya kucheza dhidi ya Seychelles katika mechi yao ya marudio siku ya Jumatatu. Kenya iliichapa Seychelles mabao 11-0 na inahitaji sare pekee ili kusonga mbele hadi raundi ya pili ya michuano ya kufuzu Olimpiki. Oduor aliwapumzisha wachezaji tegemeo kama vile Corazon Aquino, Jentrix Shikangwa na kipa chaguo la kwanza Lilian Awuor ili kuwapa nafasi wachezaji wa humu nchini. Mshindi wa jumla atakabiliana na Zimbabwe au Malawi katika raundi inayofuata.
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Mombasa, Kilifi na Malindi.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.