Mechi kati ya AFC Leopards na Bandari FC sasa itachezwa katika Uwanja wa Ulinzi Sports Complex Jumapili, ikianza saa kumi jioni. Hii ni kutokana na kutopatikana kwa uwanja uliopangwa awali, Uwanja wa Nyayo, ambao utatumika kwa mashindano ya raga ya Safari Sevens kuanzia jioni ya leo hadi Jumapili. Wakati huo huo, mabingwa watetezi Gor Mahia wataanza kampeni yao ya kutetea taji dhidi ya Murang’a Seal Jumanne katika Uwanja wa Nyayo, mechi ikitarajiwa kuanza saa moja usiku. Hii itakuwa mechi ya kwanza msimu huu kuchezwa chini ya taa za uwanjani baada ya zaidi ya miaka 19.



Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Makindu, Mtito andei na Voi.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.