Wakulima katika Kaunti ya Kirinyaga wanapunguza gharama za uzalishaji na kuboresha upatikanaji wa mbegu na miche bora kufuatia kuanzishwa kwa kituo cha kuzalisha miche kinachosimamiwa na kaunti. Kituo hicho, ambacho kilianza kufanya kazi mwaka uliopita, huzalisha miche iliyothibitishwa, isiyo na magonjwa na ya bei nafuu, jambo linalowasaidia wakulima wa mazao ya bustani kupunguza utegemezi wao kwa vitalu vya watu binafsi na vyanzo vya gharama kubwa nje ya kaunti. Kikiwa kimeanzishwa chini ya mpango wa Gavana Anne Waiguru wa 'Wezesha Kirinyaga', kituo hicho kina uwezo wa kuzalisha hadi miche elfu 400 ya mazao mbalimbali yakiwemo nyanya, kabichi, sukuma wiki, mchicha na mnavu.


 VOX POP – FARMERS