Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, anasema huu ni mwanzo tu wa mafanikio ya klabu hiyo baada ya kutia saini mkataba mpya utakaomfanya aendelee kuinoa timu hiyo hadi mwaka 2030. Mkataba wa awali wa kocha huyo raia wa Uhispania ulitarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu; sasa, muda wake wa kuiongoza 'The Gunners' unaweza kufikia muongo mmoja tangu alipoanza kazi hiyo mwezi Disemba 2019. Mkataba huo mpya unajumuisha nyongeza ya mshahara kutoka ule wa sasa wa pauni milioni 10 kwa mwaka, pamoja na bonasi ya ziada ya pauni milioni 5.
Wakati huo huo, Declan Rice yuko katika hatua za mwisho za kukubaliana na Arsenal kuhusu mkataba mpya wa muda mrefu, huku mazungumzo hayo yakiwa yamefikia hatua ya juu. Kiungo huyo wa Uingereza amekuwa mchezaji muhimu sana kwa 'The Gunners' tangu alipojiunga nao akitokea West Ham kwa ada ya pauni milioni 105 mwezi Julai 2023. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ameichezea Arsenal mara 165 na kuisaidia timu hiyo kuhitimisha ukame wa miaka 22 bila taji la Ligi ya Primia msimu uliopita. Rice anatarajiwa kupata nyongeza kubwa ya mshahara kutoka ule unaokadiriwa kuwa pauni elfu 240 kwa wiki anaolipwa sasa.
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Nairobi, Kajiado na Narok.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.