Timu ya Harambee Starlets itakosa huduma za wachezaji watatu muhimu katika mechi ijayo ya kufuzu Olimpiki dhidi ya Seychelles. Hii ni baada ya wachezaji wa klabu ya Police Bullets—Terry Engesha, Lorna Nyabuto, na Faith Mboya—kuondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa. Kulingana na klabu hiyo, walipokea taarifa rasmi kutoka FKF likielekeza wachezaji hao watatu kutoripoti kambini mwa timu ya taifa. Sababu ya agizo hilo bado haijawekwa wazi. Starlets itachuana na Seychelles kesho katika mechi ya kufuzu Olimpiki itakayofanyika katika Uwanja wa Nyayo.

 

Jaribio la Senegal la kutaka kurejeshewa taji la AFCON la mwaka 2025 litawasilishwa mbele ya Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) jioni hii. Awali, timu ya 'Lions of Teranga' ilishinda fainali ya AFCON ya 2025 kwa bao 1-0 katika muda wa nyongeza dhidi ya wenyeji Morocco jijini Rabat. Hata hivyo, baadaye CAF iliamua kuwa Senegal ilipoteza mechi hiyo na kuhesabiwa kufungwa mabao 3-0, kwa sababu wachezaji wake walitoka uwanjani kwa hasira na malalamiko wakati wa tukio la penalti. CAF iliondoa taji hilo kutoka kwa Senegal na kulikabidhi Morocco, lakini Senegal ilikata rufaa katika mahakama ya CAS mwezi Machi.




Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Kakamega, Kisumu na Eldoret.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.