Beki wa zamani wa Tottenham Hotspur, Ramon Vega, anasema anakusudia kugombea urais wa FIFA katika uchaguzi wa mwaka ujao. Mchezaji huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 55 ndiye mtu wa kwanza kuthibitisha nia yake ya kumpinga Gianni Infantino, ambaye amepuuza wito wa kujiuzulu kufuatia mpango wake ulioshindwa wa kuuza hisa za Kombe la Dunia kwa wawekezaji binafsi—hatua iliyozua malalamiko makubwa katika ulimwengu wa soka. Vega, ambaye aliwahi kucheza kama beki wa kati nchini Uswisi na pia kuichezea Celtic na Watford, amekuwa akifanya kazi katika sekta ya fedha tangu alipostaafu soka mwaka 2004.




Anga kavu vinashuhudiwa Gilgil, Nakuru na Nyahururu.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.