Harambee Starlets itachuana na Seychelles katika mechi ya mkondo wa kwanza wa kufuzu kwa Olimpiki kwenye Uwanja wa Nyayo jioni hii, huku kocha mkuu mpya Geoffrey Solo Oduor akiongoza timu hiyo kwa mara ya kwanza. Solo, ambaye alichukua nafasi ya Beldine Odemba, anasema atawatumia zaidi wachezaji wa ndani, huku wachezaji wanaocheza nje ya nchi—akiwemo Jentrix Shikangwa na Korazon Aquino—wakijumuishwa kikosini. Mechi hiyo itaanza saa tisa alasiri, na mkondo wa pili umepangwa kufanyika wiki ijayo katika uwanja huo huo. Huyu hapa Oduor.



Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Machakos, Kibwezi na Kitui.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.