Rais William Ruto amesema kufikia mwisho wa mwaka huu, wanafunzi milioni 1.3 watakuwa wamejiandikisha katika taasisi za mafunzo ya kiufundi, kutoka elfu 300 mwaka wa 2022. Akizungumza wakati wa kufuzu kwa wanafunzi 3,700 katika Mamlaka ya Kitaifa ya Mafunzo ya Viwanda NITA, Ruto alisisitiza jukumu la elimu ya kiufundi katika kuendesha utengenezaji. Aliwasihi Wakenya kubadilisha mtazamo wao kuhusu mafunzo ya ufundi.


WILLIAM RUTO-SKILLS