Anastasia Mwele, mama yake mhubiri Paul Mackenzie—mtuhumiwa mkuu katika kesi ya vifo vya Shakahola na Kwa Bi Nzaro—anasalia mikononi mwa polisi akisubiri kufikishwa mahakamani. Maafisa wa upelelezi walimkamata huko Malindi baada ya kuwaokoa wajukuu wake wanane, wenye umri wa kati ya miaka sita na 14, ambao inadaiwa walizuiliwa kwenda shule na kulazimishwa kufunga kula kwa muda mrefu. Mwele anakabiliwa na mashtaka yanayohusiana na ukatili dhidi ya watoto, mateso, na kuwanyima watoto haki yao ya kupata elimu. Huyu hapa ni Dan Mackenzie, mwanawe Paul Mackenzie, ambaye alitoa taarifa kwa mamlaka husika.


DAN MACKENZIE – ARREST