Waziri wa Usalama Kipchumba Murkomen ameseama hakuna fidia kwa mifugo iliyouawa wakati wa operesheni ya hivi majuzi ya usalama katika Kaunti ya Samburu. Akifika mbele ya kamati ya usalama bungeni, Murkomen alisema serikali kwa sasa haina mfumo wa kisheria au sera unaoruhusu Huduma ya Polisi ya Kitaifa kuwalipa fidia waathiriwa wa uhalifu. Alipinga ripoti kutoka kwa viongozi kutoka eneo hilo kwamba zaidi ya mifugo 700 waliuawa akisema rekodi rasmi za polisi zinaonyesha takriban wanyama 247 waliuawa kwa kupigwa risasi.
KIPCHUMBA MURKOMEN – RECKLESS
Wakati huo huo kundi la walalamikaji wakiongozwa na Gavana wa Samburu Lati lelelit linasisitiza fidia lazima itokee.
LATI LELELIT - FIDIA