Wanawake wanaoendelea kuvuja damu kwa zaidi ya wiki moja baada ya mimba kuharibika katika miezi mitatu ya kwanza wanashauriwa kutafuta huduma za matibabu. Mwanagainakolojia Wycliffe Musalia, anasema kuwa kuvuja damu kunapaswa kukoma ndani ya siku mbili hadi saba, huku mimba zinazoharibika katika miezi mitatu ya pili zikihitaji huduma ya hospitali ili kuhakikisha kuwa mfuko wa uzazi unasafishwa kikamilifu. Anaongeza kuwa matibabu hutegemea hatua ya ujauzito.
WYCLIFFE MUSALIA - BLEEDING