Serikali inaharakisha kukamilishwa kwa barabara zenye urefu wa mamia ya kilomita katika Kaunti ya Kiambu, zenye thamani ya Shilingi bilioni 152, ili kuboresha uchumi wa eneo hilo; haya yamesemwa na Naibu Rais Kithure Kindiki. Kindiki alieleza kuwa fedha hizo zimetengwa kwa ajili ya miradi ya barabara yenye urefu wa kilomita 1,656 ambayo iko katika hatua mbalimbali za ukamilishaji katika kaunti hiyo, huku akifichua mipango ya kina ya kujenga Barabara Kuu ya Thika-Nairobi kama alivyoahidi Rais Ruto.

 

KITHURE KINDIKI – KIAMBU