Chama cha Madereva wa Malori nchini kinasema kuwa ukosefu wa nidhamu barabarani na muundo duni wa barabara vinachangia idadi kubwa ya ajali kwenye barabara za Kenya. Katibu Mkuu Dennis Kilea anasema ukosefu wa nidhamu unawaathiri madereva wote, akibaini kuwa madereva wengi wa malori hupata mafunzo kuhusu nidhamu ya kutumia njia sahihi barabarani na hufanya kazi kwa mfumo wa zamu pamoja na mapumziko ya mara kwa mara ili kuepuka uchovu. Anasema takriban asilimia 90 ya madereva wa malori wana nidhamu na mara chache sana hupita magari mengine.


DENNIS KILEA-CRASHES