Naibu Rais Kithure Kindiki ametangaza mipango ya kuwakutanisha viongozi wa kisiasa kutoka eneo lote la Mlima Kenya kwa lengo la kukomesha vurugu za kisiasa na mivutano inayoongezeka eneo hilo. Akizungumza huko Banana katika eneo bunge la Kiambaa, Kindiki alisema mkutano huo utawakutanisha wanasiasa kutoka vyama mbalimbali ili kukubaliana kuhusu njia za amani za kutafuta kura na kunadi sera zao. Alisema hatua hiyo inafuatia jukumu alilopewa na wazee kutoka jamii za GEMA la kusaidia kukuza amani na umoja.