Waziri wa Afya Aden Duale amepuuzilia mbali uwezekano wa kufunga mipaka ya Kenya au kuwabagua watu kutoka nchi zilizoathiriwa na Ebola, kufuatia kisa cha kwanza kuripotiwa nchini humu. Akizungumza katika kipindi cha televisheni cha asubuhi, Duale alisema badala yake serikali itaimarisha miundombinu ya uchunguzi na upimaji katika vituo vyote vya kuingilia nchini. Aliwahimiza Wakenya kuepuka kusalimiana kwa mikono, kukumbatiana na maeneo yenye msongamano wa watu, pamoja na kunawa mikono mara kwa mara kwa sabuni ili kuzuia maambukizi.


ADEN DUALE – CLOSE