Mwenyekiti wa EACC, Askofu David Oginde, anasema kuwa mapambano dhidi ya ufisadi hayawezi kuachiwa tume hiyo pekee. Askofu Oginde anasema kila taasisi na kiongozi lazima wawajibike katika kukuza maadili na uadilifu. Anasema EACC hufanya mapitio ya mifumo na tathmini ya hatari za ufisadi, huchunguza sera na taratibu, na kupendekeza mageuzi ili kuimarisha udhibiti, uwajibikaji na utoaji wa huduma. Anasema taasisi lazima ziandae mipango yao wenyewe ya kuzuia ufisadi.
DAVID OGINDE – CORRUPTION