Bingwa wa London Marathon ya mwaka 2022, Amos Kipruto, na bingwa mara mbili wa Boston Marathon Sharon Lokedi, watakuwa kivutio kikubwa wikendi hii huku wakiongoza jitihada za Kenya katika Chicago Marathon. Hata hivyo, Kipruto anakabiliwa na changamoto kubwa kutoka kwa bingwa mtetezi wa Uganda, Jacob Kiplimo; Mkenya huyo akiwa na nia ya kudhihirisha ubabe wake dhidi ya mpinzani wake wa ukanda huu kufuatia matokeo ya mbio za mwaka jana. Katika Chicago Marathon ya mwaka uliopita, Kiplimo alishinda kwa muda wa saa 2:02:23, akimwacha kwa mbali Kipruto aliyemaliza wa pili.
Jua linashuhudiwa Naivasha, Gilgil na Nakuru.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.