Betika imesisitiza tena ahadi yake ya kukuza vipaji vya michezo mashinani kufuatia kuhitimishwa kwa mafanikio kwa toleo la nane la Mashindano ya Soka ya Jeff Kuria katika Uwanja wa Ruthigiti, Kikuyu, Kaunti ya Kiambu. Mashindano hayo yaliwakutanisha timu 16 katika makundi ya wanaume na wanawake, huku Barcelona FC ikiibuka bingwa katika kundi la wanaume baada ya kuifunga Wazee bao 1-0 katika fainali. VSRI ilitwaa ubingwa wa wanawake baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Musiengen. Washindi walipokea KSh elfu 100 huku washindi wa pili wakijipatia KSh elfu 50 kila mmoja.
Jua linashuhudiwa Machakos, Kibwezi na Kitui.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.