Aak-GROW na Baraza la Maua nchini wametia saini makubaliano ya miaka mitatu ya kukuza uthibiti wa wadudu kwa uwajibikaji na uendelevu wa mazingira katika tasnia ya maua nchini Kenya. Ushirikiano huo utaboresha utunzaji, uhifadhi na utupaji wa bidhaa za kudhibiti wadudu, kwa kuzingatia vyombo vitupu vya dawa za kuua wadudu. Mkurugenzi Mtendaji wa Aak-GROW Joel Mutai anasema uthibiti wa wadudu kwa uwajibikaji unazidi kuchagua bidhaa, kunahitaji utunzaji na utupaji sahihi, huku ukisaidia wakulima kukidhi mahitaji ya mazingira.


JOEL MUTAI – PARTNERSHIP