Mabingwa Ureno wamekuwa timu ya kwanza kufuzu kwa robo fainali ya ligi ya Uefa Nations kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Norway huko Porto jana usiku. Joao Cancelo aliwasawazishia Wareno dakika ya 38, dakika mbili tu baada ya Kristofer Ajer kuwaweka Wanorwe kifua mbele. Goncalo Ramos alifunga bao la ushindi dakika ya 79 na kuishuhudia Ureno ikiendelea kuongoza kundi A4 ikiwa na pointi 12, sita mbele ya Denmark ambayo iliishinda Wales inayoshika nafasi ya tatu kwa mabao 2-0.

 

Wakati huo huo, Uholanzi iliishinda Serbia 2-1 na kusogea kileleni mwa kundi A2 huku Ugiriki ikiwa na pointi 8, baada ya Wagiriki hao kutoka sare ya 0-0 na Ujerumani. Mechi nyingine za siku ya nne zilishuhudia vinara wa kundi G wakitoka sare ya 1-1 na Kosovo ilnayoshika nafasi ya pili, huku Ireland ikitoka sare ya 1-1 na Israel, na Malta ikiishinda Andora 1-0. Mechi hizo zinaendelea usiku wa leo, huku Ufaransa ikipambana na Ubelgiji, nayo Italia ikikabiliana na Uturuki katika kundi A.



Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Nairobi.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.