Kariobangi Sharks imepinga uamuzi wa FKF wa kuhamisha hadi Uwanja wa Ulinzi Sports Complex mechi yao ya marudio ya mchujo wa KPL dhidi ya Mombasa United iliyopangwa kufanyika kesho. Klabu hiyo imeeleza wasiwasi wake kuhusu mabadiliko hayo ya uwanja, ikizingatiwa kuwa awali mechi hiyo ilipangwa kuchezwa katika Uwanja wa Police Sacco. Sharks inahisi kuna njama za siri nyuma ya uamuzi wa kuhamisha mechi hiyo Ulinzi, na inasisitiza kuwa itacheza katika uwanja wa Police Sacco. Sharks itakuwa ikijaribu kubadili matokeo baada ya kufungwa mabao 2-1 wiki iliyopita, huku mshindi wa jumla akipata nafasi ya mwisho ya kushiriki KPL.
Jua linashuhudiwa Makindu, Mtito andei na Voi,
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.